Usimamizi wa kidaktari kwa wafugaji

Kwa wafugaji wanaotumia vyakula vyetu wanapewa huduma bure na madaktari wetu, Wakati wa vifaranga mpaka kuku wanaanza kutaga daktari wetu atafika shambani kwa mfugaji kila mwisho wa wiki kwa ajili ya kupima kuku uzito na kuangalia hatari zozote za kimagonjwa au kimanzigira zinaweza kuathiri ukuaji sahihi wa kuku. Baada ya kuanza kutaga daktari wetu atafika shambani kila baada ya siku 10-14 kuangalia maendeleo ya kuku.

 

Madaktari wetu watakutengenezea group maalumu la whatap ambalo litarahisisha upatikanaji wa taarifa za shambani. Wajumbe wa group ni timu ya madaktari wetu, uongozi wetu, mfugaji pamoja na kijana wa shamba. Kijana wa shamba atareport kila siku kwenye group utagaji wa siku, kuku wagonjwa, vifo, ulaji wa chakula na jambo lolote aliloliona kwa siku hyo. Hii inawasaidia madaktari wetu kupata taarifa haraka za shambani kwa mfugaji kwa ajili ya kutoa huduma za dharura (Emergence flying doctors service)

 

Madaktari wetu pia wanawasaidia wafugaji shughuli mbalimbali za kitaalamu bila malipo kama vile kuchambua kuku wasiotaga, kufanya tafiti juu za tatizo sugu shambani, kupeleka sampuli maabara za serikali kama kuna tatizo sugu n.k